May 16, 2017
Rais Magufuli ameivunja rasmi mamlaka ya ustawishaji makao makuu Dodoma(CDA)
Leo
May 15, 2017 Rais Magufuli ameivunja rasmi Mamlaka ya Ustawishaji Makao
Makuu Dodoma (CDA) na kuagiza mali na shughuli zote zilizokuwa
zikifanywa na CDA zihamishiwe Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
Rais
ameivunja CDA kwa kutia saini hati ya Amri ya Rais ya kuivunja Mamlaka
hiyo Ikulu Dar es Salaam, tukio ambalo limeshuhudiwa na Makamu wa Rais
Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Majaliwa, Waziri wa Ardhi William
Lukuvi.
Wengine
ni Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba, Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Antony Mavunde, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Jordan Rugimbana na viongozi mbalimbali wa wizara.
Rais
Magufuli amesema ameamua kuivunja CDA na kuhamishia majukumu yake
katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ili kuondoa mgongano wa utoaji
wa huduma uliokuwa ukisababishwa na vyombo hivyo viwili na pia kuendana
na mahitaji ya sasa ambayo yamedhihirisha kuwa hakuna haja ya kuwepo kwa
CDA.
Kufuatia
uamuzi huo Magufuli pia ameivunja Bodi ya CDA, aliyekuwa Mkurugenzi
Mkuu wa CDA Eng. Paskasi Muragili atapangiwa kazi nyingine na ameagiza
wafanyakazi wote wa Mamlaka hiyo wahamishiwe Halmashauri ya Manispaa ya
Dodoma na ofisi nyingine za Serikali kadiri inavyofaa.

















VIDEO: Katika hili lazima nimshukuru Rais Magufuli’ – Maftaha Nachuma. Tazama hapa chini
May 12, 2017
Subscribe to:
Posts (Atom)